Ile harusi ya mastar wawili wa Bongo Flava iliyokuwa ikisubiriwa na wengi kati ya mzee wa kiduku Marlaw na mwanadada Besta hatimaye ilifanyika kwa siri mwishoni mwa wiki jijini A-Town (Arusha) huku ikiwa na ulinzi wa wa kufa mtu uliowazuia mapaparazi kuweza angalau kufotoa vijisnepu.
Taarifa za uhakika toka ndani ya jiji hilo zinamimina kuwa harusi hiyo ilifanyika katika Kanisa Katoliki Moshono nje kidogo ya Jiji la Arusha, gari walilotumia maharusi hao kwenda kanisani halikuwa limepambwa kama ilivyo desturi ya harusi nyingi.
Mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, kulifuatiwa na zoezi la upigaji picha kwa maharusi hao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha, ikiwemo Hoteli ya kitalii ya Kibo Palace. Wakati huo, umakini wa walinzi wa maharusi hao uliongezeka kuhakikisha hakuna Paparazi anayewasogelea mastaa hao.
Hatimaye, maharusi waliwasili katika Hoteli ya Golden Rose saa 2:50 usiku huku wapambe wakiwa macho kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. Kilichojiri katika harusi hiyo ni uchache wa watu walioalikwa tofauti na ilivyotazamiwa kutokana na umaarufu wa maharusi hao.
Marlaw na Besta walitinga katika hoteli hiyo kwa tahadhari kubwa. Baada ya kuteremshwa umbali wa mita 50 kutoka kwenye lango la ukumbi wa sherehe, walipakizwa ndani ya teksi bubu yenye namba za usajili T 220 AWP, Toyota Premio na kuwafikisha hadi ukumbini.
Marlaw alikuwa amevalia suti nyeusi na shati jeupe, huku Besta akiwa amevaa shela jeupe alilokuwa amelishikilia lisiburuzike chini.
Baada ya kuteremka ndani ya gari, walinzi wa maharusi hao waliwazingira huku wakihaha kuwapitisha kwa kuhofia wasipigwe picha na mapaparazi waliokuwa eneo hilo wakiwawinda kama mbwa mwitu.
Walinzi hao walifanikiwa kuwavusha maharusi kwa kutumia uchochoro wa hoteli huku wakitahadharisha kwamba mtu yeyote asithubutu kuinua kamera yake juu kwa lengo la kupiga picha.
Harusi hiyo ilionekana kupooza kwa kiwango kikubwa kutokana na uchache wa watu. Wageni walioalikwa walikadiriwa kufikia 30 au 40, ambao walishindwa kutoa ushirikiano wa kupiga vigelegele katika ukumbi huo. Walinzi walikuwa wengi pamoja na wale wa hoteli hiyo waliohakikisha kwamba hakuna ‘mzamiaji’ mwenye kamera.
Katika sherehe hiyo, nyimbo za Marlaw ndizo zilizotawala kuwatumbuiza waalikwa hao wachache. Hakukuwa na msanii au mtu yeyote maarufu aliyealikwa kwenye harusi hiyo, hali iliyowashangaza wengi.
“Hivi kweli Marlaw hana marafiki? Mbona hatuwaoni watu wengine maarufu?” Alihoji mwalikwa mmoja.
Wakati harusi ikiendelea, mtu mmoja alizamia ndani ya ukumbi wa sherehe hiyo, akadhaniwa ni paparazi. Walinzi wa Marlaw walimfuata na kumzingira, wakamshushia kipigo huku wakidai kwamba ametumwa kupiga picha. Walimny’ang’anya baadhi ya vitu walivyomkuta navyo.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwa katika kamati ya maandalizi ya harusi hiyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, ameeleza usiri wa ndoa hiyo umetokana na kuwepo kwa taarifa kuwa mzazi mwenza wa Marlaw (jina halikutajwa) alikuwa akiifuatilia ndoa hiyo kwa udi na uvumba ili aweze kuzuia isifungwe.

No comments:
Post a Comment