Wednesday, March 16, 2011

BASATA kufungua ukurasa upya wa mashindano ya urembo

Litafanya mabadiliko makubwa katika mashindano yote ya Urembo hapa nchini, ili yafanyike kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo.
Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego aliyasema hayo alipokuwa kwenye jukwaa la Sanaa, litakalofanyika kila Jumatatu barazani hapo wakati walipokuwa wakihitimisha mada ya Mchango wa Mashindano ya Urembo na Mitindo katika kukuza ajira iliyokuwa ikiwasilishwa na Juliana Urio ambaye ndiye muandaaji wa Shindano la Kisura litakalofanyika kila mwaka.

Alisema kwamba Baraza linakusudia kuwaita waandaaji wote wa mashindano ya urembo na mitindo, ili kuwakutanisha na wadau mbalimbali kwa ajili ya kueleza changamoto zilizopo na baadaye kuja na mapendekezo ambayo yatafanya mashindano hayo kuwa bora zaidi.

Alisema wanatambua mchango wa mashindano hayo, lakini lazima yafanyike katika misingi iliyo wazi na yenye ubora zaidi ndiyo maana wanataka kuwaita waandaaji wote kuwakutanisha na wadau mbalimbali ili wapate changamoto na michango mbalimbali ya uboreshaji.

Aliongeza kwamba si nia ya baraza kufuta shindano lolote lakini alisisitiza kwamba, shindano linapokuwa na mapungufu mengi lazima lifutwe.

Pia lazima waandaaji wazingatie masharti na taratibu zote wanazopewa, ili kuepuka kufutwa ka mashindano hayo.

No comments: