Vikosi vya kuweka amani vya Umoja wa Mataifa na majeshi ya DRC
vimemkamata kiongozi wa waasi anayetuhumiwa kuongoza mashambulio yaliyohusisha
kubakwa kwa mamia ya raia.
Umoja wa Mataifa unasema Luteni Kanali Mayele wa kundi la waasi la Mai Mai
Cheka alikamatwa kufwatia harakati za pamoja katika mkoa wa Kivu Kaskazini.Watu kati ya 300 na 500 wanasemekana kubakwa wakati wa mapigano mashariki mwa Congo mwezi Julai na Agosti.
Vikosi vya kuweka amani vilishtumiwa kwa kushindwa kuzuia matukio hayo,ambayo mengine yalifanyika karibu na kambi ya Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment