This blog it's for people which have respect to other people.
Friday, July 30, 2010
Moi aambiwa amheshimu Kibaki
Rais wa zamani wa Kenya Daniel Arap Moi
ameambiwa na kamati ya kujenga usalama, kuwa amheshimu rais aliyeko madarakani,
kufuatia wawili hao kushambuliana kwa maneno katika moja ya kampeni kuhusu
katiba
Daniel Arap Moi, Rais wa zamani wa Kenya
Rais Mwai Kibaki anataka wananchi wa Kenya kuupitisha muswada wa katiba
mpya, huku Bw. Moi akiongoza kampeni ya kupinga katika hiyo.
Lakini kamati iliyoundwa ya kujenga utaifa imesema mzozo huo wa kibinafsi
unaathiri kazi zake.
Baadhi wanahisi Kenya
huenda ikarejea katika hali iliyotokea mwaka 2007 na 2008 baada ya kufanyika
uchaguzi ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa na wengine laki 3 kukosa
makazi.
Rais Mwai Kibaki
Siku ya Alhamisi, Bw. Moi ambaye aliwahi kuwa rais wa Kenya kwa miaka
24 alisema Bw. Kibaki hatakiwi kumshutumu kwa kupinga muswada huo, kwa kuwa
hakutimiza ahadi yake ya kubadili katika ndani ya siku 100, wakati alipoingia
madarakani mwaka 2002.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya kujenga utaifa (NCIC) Mzalendo Kibunjia
amemtaka Bw. Moi kumheshimu rais na kutoa wito kwa Bw. Moi na Bw. Kibaki
kujizuia kutoa matamshi ambayo yanaweza kusababisha mvutano katika kampeni za
kura hiyo ya maoni.
Ghasia za mwaka 2007-8
Kura ya maoni itafanyika Agosti 4.
Watu wasiopungua sita waliuawa baada ya bomu la kurushwa kwa mkono kutupwa
katika mkutano wa kampeni ya kupinga rasimu hiyo mwezi Juni mjini Nairobi, huku wabunge
watano wakishitakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki wakati wa kampeni hizo. Hatua
hiyo ilifuatua malalamiko yaliyofikishwa kwa NCIC.
Ghasia nyingi za mwaka 2007-8 zilitokea wakati uhasama katika uchaguzi
ulipozusha mizozo ya kugombea ardhi, hasa katika eneo la Bonde la Ufa, sehemu anayotoka Bw.
Moi.
Moja ya kipengele katika rasimu ya katiba mpya, ni kuunda tume ya ardhi
ambayo itataifisha ardhi iliyopatikana kwa njia zizozo halali wakati wa utawala
wa rais Moi.
No comments:
Post a Comment