Tuesday, July 27, 2010

Mchina 'mwenye manywele' kucheza filamu ya Mfalme wa Kima


Mtu "mwenye manywele", Yu Zhenhuan, anategemewa kufanyiwa upasuaji wa sura yake ili iweze kuvutia katika kuigiza kwenye televisheni.
RAIA wa China ambaye ana 'manywele' mengi zaidi mwilini anategemewa kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha mwonekano wake ili aweze kucheza katika filamu ya Mfalme wa Kima katika mchezo mmoja wa televisheni uitwao 'Safari Kwenda Magharibi'.

Mtu huyo aitwaye Yu Zhenhuan, mwenye umri wa miaka 32, ana nywele zinazofunika asilimia 96 ya mwili wake kutokana na kasoro katika homoni zake.

Zhenhuan amewahi kucheza katika filamu kadhaa,lakini mkurugenzi wake aliamua kwamba kutokana na kutokuwa na mvuto kwa watu, ilibidi afanyiwe upasuaji wa kurekebisha sura yake.

"Nilifikiri mimi ndiye mchezaji bora kuliko wote kwani ninaonekana kama kima na jina langu ni mtu-kima," alisema Zhenhuan.

Aliongeza kusema: "Nilisoma katika kitabu kimoja na nikampata fundi wa nywele ili anifanye nionekane mtu-kima wa kweli.

Lakini nilishindwa katika usaili kwani sina mwonekano mzuri.

"Nitalazimika kufanyiwa upasuaji wa kuondoa nywele hizi pamoja na marekebisho usoni ili niweze kuonekana kama kima mzuri zaidi na hivyo kumfanya mkurugenzi huyo ajutie uamuzi wake wa kuniacha," alisema Zhenhuan akizungumza na gazeti la China Youth Times.

No comments: