Saturday, July 31, 2010

KLABU YA NEWCASTLE IMEKAMILISHA KUTIA SAINI YA KUMCHUKUA MLINZI WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND SOL CAMPBELL KWA MKATABA WA MWAKA MMOJA.




Campbell alikuwa huru kuondoka baada ya mkataba wake na Arsenal kumalizika mwishoni mwa msimu wa ligi uliopita.
Lakini pia kulikuwa na taarifa kwamba Arsenal walikuwa na nia ya kuongeza muda wa mkataba na Campbell msimu unaokuja.
Taarifa za mlinzi huyo kuelekea Newcastle zinaondosha taarifa zingine zilizokuwepo kwamba huduma zake pia zilihitajika katika klabu ya Sunderland, na pia klabu ya ligi kuu ya Scotland- Celtic.
''Kujiunga na Newcastle, klabu yenye utamaduni wa kujivunia, na wafuasi wengi , bila shaka kwangu ni fahari kubwa.'' Alisema Campbell.
Anakuwa mchezaji wa tatu kuchukuliwa na meneja wa Newcastle Chris Hughton, kwa maandalizi ya klabu hiyo ya kurejea kwenye ligi ya Premier ya England, baada ya kucheza daraja la chini msimu uliopita.
Tayari Hughton alikuwa amekwishawachukua Dan Gosling kutoka Everton na James Perch kutoka Nottingham Forest.
Campbell alifunga ndoa karibuni Fiona Barrat, na punde tu baada ya kurejea kutoka fungate alikwenda kufanya majaribio ya kiafya tayari kuanza shughuli na Newcastle.
Katika msimu uliopita aliichezea klabu ya Arsenal mechi 11 baada ya kupata mkataba mfupi nao mwezi Januari.
Ilikuwa ni mara ya pili kwa Campbell kuichezea Arsenal, aliyokuwa ameiacha mwaka 2006 kujiunga na Portsmouth.
Akiwa Arsenal waliwahi kushindi taji la premier mara mbili, Kombe la FA mara tatu, na alipojiunga na Portmouth akawaongoza kutwaa taji hilo la FA mwaka 2008.
Msimu uliopita Campell alianzia kwenye ligi ndogo ya daraja la pili katika klabu ya Notts County kabla ya kuondoka kwa hiari kurejea Arsenal Septemba mwaka uliopita.
Ameshaichezea timu ya taifa ya England mara 73.

No comments: