Hakuwa mwingine bali ni yule Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema (TLP), alitoa ufafanuzi juu ya uwamuzi wake wa kutounga mkono baadhi ya uamuzi wa Chadema na ni utashi wake binafsi.
Mbunge huyo alisema amekereka na kauli ya Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Chuki Abwao (Chadema) aliyoitoa ndani ya bunge hilo siku za usoni zilizopita.
Kwani Mbunge huyo wa Viti Maalum Iringa alipokuwa akichangia mjadala wa Wizara ya Mambo ya Ndani, alisema Mrema ni kibaraka wa CCM.
Mrema alisema, hoja hiyo haina ukweli wowote na kwamba hawezi kuacha kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake, kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka na madaraka ya nchi hii, na mengi ameyafanya kwa maendeleo ya wananchi wa Jimbo la Vunjo.
“Lazima nimuunge mkono Rais wangu, siwezi pingana naye ndiyo mtu mwenye madaraka na yote nitakayo kanifanyia jimboni, wengine wasio na madaraka siwezi waunga mkono,” alisema Mrema.
Alisema, suala la yeye kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa si upendeleo, na kwamba hata wao Chadema katika Bunge la tisa, walipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya hiyo anayoishikilia yeye.
No comments:
Post a Comment