Si mwingine bali ni yule Msanii na Mtayarishaji mahiri wa Filamu kwa hapa nchini Tanzania, Yvonne Cherryl 'Monalisa', kwa juhudi zake ndizo zilizompelekea kuteuliwa kushiriki kinyang'anyiro hicho.
Kwani tuzo hizi zinatarajia kufanyika New York nchini Marekani mwezi Septemba, na anashiriki katika kipengere cha Pan Africa Actress of the Year.
Kwa tukio hili tu tayari mwanadada huyu anastaili kusaidiwa ili iwe nuru katika kuitangaza sanaa ya filamu kwa Afrika na Ulimwenguni kote.
Kwa upande wake Monalisa alisema amefurahishwa kwa kuteuliwa kwenda kushiriki kinyang'anyiro hicho, kwa sababu kuna watu wameshaanza kumpigia kura mwanadada huyo ili aweze kuibuka kidedea na ushindi mnono.
Alisema anaamini kuwa watanzania wanaweza, ni muda wao kumuunga mkono Mtanzania mwenzetu kwa ajili ya kuiletea heshima nchi yetu.
Watanzania tushirikiane kwa pamoja tumpigie kura Yvonne Cherryl, piga kura yako kupitia www.nigeriaentawards.com hapa ukiingia unakutana na picha ya Monalisa unajisajili ili uweze kumpigia kura. Mungu ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Yvonne Cherryl.
No comments:
Post a Comment