Mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi na serikali za Afrika
unaotarajiwa kukamilika hii leo mjini Kampala, Uganda umeafikiana kuongeza
majeshi zaidi nchini Somalia.
Maafisa wamesema kuwa AU imekubali kupeleka wanajeshi 2000 zaidi katika mji
mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Aidha, maafisa wa muungano huo wametangaza kuwa uwezo wa majeshi hayo huko
Somalia utabadilika, ili kuwaruhusu wanajeshi kupambana na wanamgambo iwapo
watabaini kushambuliwa.
Bado haijawa wazi wanajeshi watakaopelekwa Somalia watatoka nchi zipi. Hata
hivyo awali, mwandishi wa BBC aliyeko Kampala, Uganda ambapo mkutano huo
unafanyika, anasema awali nchi za Guinea na Djibouti zilitangaza kuwa zilikuwa
tayari kutoa vikosi vya wanajeshi wao.
Awali, rais Museveni wa Uganda alitoa wito wa kuongezwa kwa jitihadi za
kukabiliana na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Al- Shabaab. Kundi hilo
limekiri kufanya mashambulio ya Kampala, ambapo watu zaidi ya 76 walikufa,
waliposhambuliwa wakitizama fainali za kombe la Dunia za 2010.
No comments:
Post a Comment