Monday, July 12, 2010

60 WAUAWA KATIKA MILIPUKO YA BOMU UGANDA




Milipuko imetokea katika mji mkuu wa Uganda Kampala iliyolenga mashabiki wa soka waliotizama mechi ya mwisho ya kombe la dunia katika televisheni.
Idadi kamili ya waliofariki bado haijulikani japo awali miili 23 ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Duru zinaarifu kuwa idadi hiyo inahofiwa kufikia zaidi ya watu 60.
Mkuu wa polisi nchini humo Kale Kaihura amesema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa milipuko hiyo iliyotokea katika mikahawa ya vyakula na pombe ilinuiwa kusababisha maafa zaidi.

Waathiriwa wa mlipuko nchini Uganda
Shaka kuu imetiliwa kikundi cha wapiganaji wa kiislamu Al-Shabab nchini Somalia ambako Uganda imetuma majeshi yake kusaidia katika shughuli ya amani chini ya muungano wa Afrika.

No comments: