Sunday, June 6, 2010

MAMBO YANAYO TUFANYA TUWE WASWAHILI...

1.Unamwita mtu usiyemjua(wala kukutana nae kabla) aunt au uncle ama shemeji.
  

 2.Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original copies).
  

3.Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo  siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.
  
4.Una machupa ya maji matupu ya shampoo perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo.
  
5.Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali,chidi,mamu, mwanamambo, shida, dida n.k.
  

6.Ikiwa una kompyuta, asilimia 99 ya programu ulizonazo ni 'pirates' na hakuna 'genuine' hata moja, na japo unazo, zinakotengenezwa ama bei zake hujui.
  
7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k  ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani.
  

8.Rafiki yako anapokuwa na mgogoro na mpenzi wake unatamani kisiri-siri waachane ili umchukue shemeji yako, japo unajidai kuwapatanisha kwa bidii sana .
  

9.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano  usiku sana )na mara nyingi huwa una beep tu.
  
10.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.
  

11.Wakati ukisafiri japo una nauli kamili unatamani konda asahau kukudai ama umlipe pungufu ya nauli ya kawaida.
  
12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi  asingekuwa vile yule.
13. Ualikwapo kwenye sherehe au mkutano hufika baada ya muda ulopangwa kupita waweza zidisha hata masaa mawili mbele au zaidi.
14. Unapokuwa kwenye sherehe hutaki kuchukuliwa 'moving' iwapo kuna video inayotengenezwa.
15. Kudhihirisha kama wewe ni mswahili ukimaliza kusoma hii email lazima utabisha tu na kunimaindi… Lazima uchonge

No comments: